USAJILI WA KAMPUNI
Kampuni ni nini?
Kampuni ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye nia ya kufanya biashara halali na kuusajili mjumuiko huo chini ya Sheria ya kampuni.
Aina za Kampuni
Kampuni ya kigeni
Kampuni binafsi
Kampuni ya umma
Faida za Urasimishaji Kampuni ni zipi?
Kuipatia utu wa kisheria biashara yako
Kutambulika na taasisi za fedha mf. bienki wakati wa kufungua akaunti.
Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
Kupanua wigo wa kufanya biashara kubwa, mf. biashara za kimataifa
Urahisi wa kuitangaza kampuni kwa urahisi na kupanua wigo wa wateja.
Vigezo vya kusajili Kampuni
Mwombaji anatakiwa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA
Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA ya kila mwanahisa
Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA au pasi ya kusafiria kwa raia wa kigeni na namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) ya kila mkurugenzi
Nyaraka za kuambatisha
Katiba ya Kampuni
Fomu ya uadilifu
Fomu ya majumuisho (Consolidated Form)
Hatua 10 za kusajili Kampuni
Tembelea "www.brela.go.tz" au "ors.brela.go.tz".
Ingia katika akaunti yako ya Usajili kwa njia ya mtandao (ORS) au tengeneza akaunti katika mfumo.
Chagua "huduma mtandao".
Chagua "kampuni".
Chagua "aina ya huduma".
Chagua "aina ya kampuni".
Jaza taarifa za kampuni husika.
Pakia viambatisho katika mfumo.
Lipa kwa njia ya simu au benki.
Maombi yatafanyiwa kazi baada ya malipo kupokewa.
Tags:
BIASHARA