Mhe.Gekul awaongoza Watanzania Kutazama Royal tour, Kombe la Dunia, Dkt. Abbasi achana mistari





Na John Mapepele

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul leo Juni 1, 2022 amewaongoza watanzania kuangalia Filamu ya Royal Tour,   kushuhudia na kupiga picha  na Kombe la Dunia la FIFA katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mhe. Gekul ameambatana na Mwenyekiti wa Kamati  ya kuitangaza Tanzania ya Royal Tour ambaye pia ni Katibu Mkuu wizara hiyo  Dkt. Hassan Abbasi na watendaji wa sekta ya michezo nchini.


Akizungumza  kabla ya kuanza kutazama Filamu ya Royal Tour, Mhe. Gekul amewapongeza Coca Cola kwa  kudhamini ujio wa kombe hilo nchini.

Ameongeza kuwa ujio wa Kombe hilo ni ishara  kuwa FIFA inathamini jitihada zinazofanywa na Serikali kwenye Michezo.

Amesema kwa sasa Serikali inakusudia   kuanzisha  vituo vya michezo na kurudisha Kombe la Taifa ambalo linakwenda kuibua  vipaji.


Wasanii mbalimbali wakiongozwa na Sholo Mwamba  wametumbuiza wakati Dkt. Abbasi pia akichana mistari na kuwashangaza  wapenzi wa hip hop waliokuja kushuhudia kombe na kutazama Royal tour.


Post a Comment

Previous Post Next Post