FCC, ZFCC ZAJIPANGA KUDHIBITI UINGIZAJI WA BIDHAA BANDIA ZANZIBAR NA TANZANIA BARA



Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) William Erio ( Wa Kwanza Kulia)  akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara ya kikazi ya siku tatu iliyofanywa na Tume halali ya ushindani Zanzibar ya kutembelea   FCC ikiwa na lengo la kuimarisha mahusiano na kuangalia namna bora ya kutekeleza majukumu yao. (Katikakati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali ya biashara Mohammed Sijari Mohammed  na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi muungano ya makampuni na udhibiti wa ushindani,  ZFCC Bi Ummi Mohammed Rajab) 



Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali ya biashara Zanzibar Mohammed Sijari Mohammed akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu iliyofanywa na Tume halali ya ushindani Zanzibar ya kutembelea   FCC Tanzania Bara. 

PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI 



Tume ya ushindani FCC kwa kushirikiana na Tume ya ushindani halali ya Zanzibar Zfcc zimejipanga kudhibiti uingizaji na uzalishajwi wa bidhaa bandia ili kuchochea uchumi utakaolinda soko la ndani na Kumlinda mlaji 

Ameyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) William Erio hapo jana wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu kwaajili ya kutembelea  Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) ikiwa na lengo la kuimarisha mahusiano na kuangalia namna bora ya kutekeleza majukumu yao


"Suala la bishara  si suala la muungano, kwahiyo sisi FCC tunashughulika na masuala haya ya kibiashara kwa maana ya kushajihisha ushindani, kulinda washindani katika shughuli zao na kumlinda mlaji kwa Tanzania bara ambapo na wenzentu wanafanya hivyohivyo kwa upande wa Tanzania Zanzibar"

"Pamoja na kwamba suala la biashara si suala la muungano lakini muingiliano kibiashara kati ya pande hizi mbili za muungano ni mkubwa  kwanza kwa wafanyabiashara wenyewe lakini pia wawekezaji ambao wamewekeza katika pande zote mbili za muungano"


Aidha Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya awamu ya sita imejikita katika kuimarisha uwekezaji Kama njia mojawapo Kuu ya kuleta mitaji na kukuza uchumi wa nchi yetu Kama vile inavyofanya serikali ya awamu ya nane kule Tanzania Zanzibar.

Pia Erio alisema wanajipanga zaidi katika kuhakikisha kwamba nchi yetu inanufaika na soko la Afrika Mashariki kwasababu sisi wote ni sehemu ya Afrika mashariki.

Kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali ya biashara Mohammed Sijari Mohammed amesema  kuwa Zanzibar inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya mapitio ya baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya maendeleo ya viwanda ambayo itawezesha wananchi kunufaika  na bidhaa zinazozalishwa viwandani.


"Kwa upande wa Zanzibar kuna jitihada kubwa zinafanyika za makusudi kwake Mhe. Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuweka mazingira bora ya biashara na kudhibiti ushindani"
 
Aidha Sijari alisema 
Kuna sheria nyingi wanazifanyia mapitio mfano sheria ya maendeleo ya viwanda ambapo wameamua kuwepo kwa sheria hiyo.

Miongoni mwa mambo ambayo ZFCC imejifunza kutoka Tume ya Ushindani Bara ni pamoja na masuala ya ukaguzi na udhibiti wa bidhaa bandia ,taratibu za kanuni na sheria ,na masuala ya muunganiko baina ya kampuni.

Post a Comment

Previous Post Next Post