Na
Mwandishi Wetu
Wazazi
na walezi wanaowapeleka watoto katika shule za bweni wakiwa bado wadogo
wameshauriwa kuwafuatilia kwa karibu katika makuzi yao wakiwa shuleni na wakati
wa likizo, ili kuwaepusha na wimbi la vitendo vya ukatili wa kijinsia katika
ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Aidha,
amepiga marufuku suala la watoto kubebwa kwenye bodaboda, akisema ni hatari kwa
usalama wao, na kwamba yeyote atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Katibu
tawala huyo amebainisha hayo jana katika sherehe za mahafali ya nne ya Watoto
waliohitimu elimu ya awali katika shule ya Kimataifa ya Monti iliyopo Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
“Kama
serikali tunawakumbusha wazazi umuhimu wa kuwa karibu na watoto wao kwa sababu
ukiangalia dunia inavyokwenda, tunahitaji mawasiliano ya karibu kati ya mzazi
na mwalimu anayemwangalia mtoto akiwa shuleni, pamoja na kujua wanachanganyika
na watu gani wanaporudi nyumbani,” amesisitiza Warda huku akiipongeza Shule ya
Kimataifa ya Monti kwa kuibua na kulea vipaji vya watoto ili kuendana na
mabadiliko ya kiteknolojia katika dunia ya sasa.
Pia
ameeleza kufarijika na malezi pamoja na elimu ya kisasa wanayopatiwa watoto hao
na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na uongozi wa shule hiyo
inayotumia mtaala wa kimataifa wa Cambridge unaozingatia kiwango cha kimataifa
cha elimu na kutambuliwa na vyuo vikuu na waajiri kote duniani.
Akizungumzia
mahali hayo, Mkurugenzi Mkuu na mmiliki wa shule hiyo, Fatma Fernandes amesema
shule hiyo inampokea mtoto mwenye umri kuanzia mwaka mmoja na kuendelea kisha
kumlea na kumkuza kielimu hadi anapofikisha umri wa miaka mitano ndipo
anapoanza darasa la kwanza.
“Kwa
elimu ya msingi watoto wanasoma kwa miaka sita. Shule ina matarajio makubwa
ikiwemo kujenga miundombinu inayolenga kuunga mkono vipaji vya watoto. Mfano
tunajenga ‘swimming pool’ kwa wale wanaopenda kujifunza kuoegelea, pia
tutajenga viwanja vya mchezo wa mpira wa kikapu na tenesi, pia tunajenga
kampasi Madale ambayo itakuwa ya msingi na sekondari na ni kutwa na bweni,”
amesema.
Aidha,
amesema wamejikita kuhakikisha watoto wanasoma kompyuta kupitia maabara ya
kompyuta iliyopo shule hapo.
“Kuhusu
matumizi ya AI hatujaangalia tu kwa mtoto lakini pia tumeangalia pia kwa
mwalimu ili kurahisisha kazi ya ufundishaji. Kwa sasa kuna School AI ambayo
tumeweka kwenye mifumo yetu ambayo inamsaidia mwalimu kumrahisishia kutengeneza
mpango kazi wa masomo, mwalimu hatumii tena saa 40 kama zamani, kwa muda mfupi
anaweza kutengeneza kila kitu anakwenda darasani na kuwafundisha watoto na
kumuelewa,” amesema na kuongeza;
“Walimu
wamejikita kuelewa AI na kuhakikisha watoto wetu wanaitumia kwa usalama.
Kompyuta zetu zote zina mifumo ambayo ni salama kwa watoto kutumia”.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi wenye watoto shuleni hapo, Kaley Milao alieleza kuridhishwa na uwezo wa watoto walionesha katika masomo pamoja na kufikiri.
“Tunategemea makubwa kwani wanafungua kampasi kule Madale. Utakuwa ni muendelezo mzuri kwa sababu AI au teknolojia haiepukiki, lazime tuende nayo tuone namna gani tunaitumia kutufaidisha sisi,” amesema.