Vyombo vya habari vya Serikali vimetakiwa kuhakikisha vinatoa nafasi sawa ya kuripoti habari kwa vyama vya siasa katika kipindi cha uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Rai hiyo umetolewa leo Mei 02/2025 na Wakili na Mshauri Wakili wa Mahakama kuu, Mh.Lwijiso Ndwela wakati mahojiano Waandishi nguli wa habari kwenye mjadala ujulikanao kama "Cafe Talk" ulioandaliwa na Clouds Media, kwa kushirikiana na Crown Media pamoja na Ayo Tv ikiwa ni kuzungumzia kanuni mbalimbali za uchaguzi zinazosimamiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Wakili Ndelwa amesema kuwa kanuni za uchaguzi zinaelekeza vyombo vya habari vya imma kama vile TBC, kutoa nafasi sawa ya kuripoti taarifa ya vyama vya siasa ikiwemo kwenye mikutano ya hadhara,mahojiano maalumu pamoja na mambo mengine ili kuweka usawa wa utoaji wa taarifa kwa vyama hivyo.
"Kanuni hizi za uchaguzi zinatoa maelekezo mbalimbali wakati wa kipindi cha uchaguzi ikiwemo kuvitaka vyombo vya habari kutoa fursa sawa kwa vyama vya siasa kutangaza taarifa zake,nasio kuendelea chama ilichopo madarakani pekee" amesisitiza Wakili Ndelwa.
Nakuongeza kuwa,"Wakati mwingine vyombo vya habari vya Serikali vimekua havitekelezi kanuni hiyo na kuendelea kufanya upendeleo kwa baadhi ya vyama jambo ambalo ni kinyume na kanuni za uchaguz