Taasisi isiyo ya kiserikali ya LALJI FOUNDATION imetoa msaada wa futari kwa wananchi takribani 200 wa Kata ya Msanga Wilaya ya kisarawe kwa lengo la kuwafikia baadhi ya waumini wa kiislamu wenye uhitaji maalumu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa LALJI FOUNDATION Ndug. Imtiaz Lalji amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwasaidia waislamu wenye uhitaji kupata futari katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya wananchi wameishukuru taasisi ya LALJI FOUNDATION, kwa msaada waliowapatia kwani msaada huo umekua ni faraja kwao katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
#ibnupdates