Veronica Simba – LindiWakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wadau wake mbalimbali mkoani Lindi, wamekubaliana kuunganisha nguvu katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.
Azimio hilo limefikiwa leo Januari 27, 2023 katika kikao kazi kilichojumuisha Ujumbe kutoka REA ukiongozwa na mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Oswald Urassa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Ngusa Samike, Ujumbe kutoka TANESCO, Wabunge wa Lindi pamoja na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani humo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Urassa amesema kikao kimekubaliana kuwa kila Mkandarasi atatakiwa kuandaa na kuwasilisha Mpango Mkakati unaodadavua namna atakavyotekeleza kazi zake kwa mlengo wa kukamilisha Mradi kwa wakati.
Akifafanua, amesema Mpango Mkakati huo utaainisha taarifa ya kila wiki na kila mwezi kuanzia sasa hadi Aprili 30 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya hitimisho kwa kila mmoja kuwa amekamilisha na kukabidhi Mradi.
Amesema Bodi ya REA itahakikisha inafuatilia kwa ukaribu na hatua kwa hatua, utekelezaji wa Mradi kwa kila Mkandarasi ili malengo ya Serikali kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya kuwapelekea huduma ya umeme wananchi waishio vijijini itimie.
“Fedha hizi ni za wananchi hivyo ni lazima zitumike kama inavyopaswa. Hivyo, ni jukumu lenu ninyi Wakandarasi kuhakikisha mnatimiza makubaliano yetu tuliyoazimia leo ya kukamilisha miradi kwa wakati,
Tags:
HABARI