WATU WENYE CHANGAMOTO YA VIUNGO KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA (NHIF)




PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI 

Serikali kupitia wizara Afya imesema kuwa imejipanga kuhakisha wanaweka utaratibu wa huduma za watu wenye changamoto ya  Viungo saidizi waingizwe katika mfumo wa Bima ya Afya (NHIF)

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na  Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Tiba kwa Hospital zote hapa nchini luteni kanali Dokta Pius  Horumpende  Wakati wa Mkutano ulio Wakutanisha wadau mbalimbali wanajishugulisha na wauzaji na utengenezaji  wa Vifaa Tiba saidizi wa watu wenye Ulemavu wa Viungo.



"amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakisha kuwa wananchi wana patahuduma hii muhimu kwa Unafuu hasa kwa watu  wenye uhitaji wa adha hiyo ya Vifaa Tiba  saidizi  vya Viungo vya  watu hao,


 Serikali itaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kutoa nafuu kwa vifaa muhimu kama hivi vya vifaa tiba Viungo Ili kuhakisha wana nchi wanapata huduma njema na wananchi kufurahia huduma za hospital zinazo tolewa hapa nchini.

Naye Rais wa chama Cha Watu wanao toa huduma ya  Vifa Tiba na Viiungo Saidizi Bi Leah Baiki .amesema kuwa mkutano huo umewakutanisha wadau tofauti wanao jihusisha na Utengenezaji na wauzaji wa Vifaa tiba vya Viungo saidizi ikiwa lengo ni kuhakisha wanapeana uzoefu na kutoa elimu kwa Jamii juu ya huduma hizo wanazo zitoa.



Ameongeza kuwa mkutano huo umeenda  na maonesho ya kuonyesha shughuri zao wanazo zitoa  kwa wananchi Ili waweze kufahamu huduma hizo sambamba na kufamiana kama wadau wa sekta hiyo muhimu katika nchi.


Post a Comment

Previous Post Next Post