VIJANA MAGU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI



Vijana katika Wilaya ya Magu  wameaswa kutumia kikamilifu fursa za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa  na halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu  (DAS), Zuberi Said Zuberi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la vijana tarafa ya Itumbili  lililofanyika katika viwanja vya sabasaba Wilayani Magu  ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025.

Katika hotuba yake, DAS aliwahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kuwachagua viongozi wanaoendana na mahitaji na maono yao. “Uongozi bora huanza na uchaguzi bora, Vijana mna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu,” alisisitiza.

Mratibu wa kongamano hilo ambaye ni Afisa maendeleo ya  vijana Wilaya ya Magu Bi. Prisca Salum   alieleza kuwa lengo kuu ni kuwaunganisha vijana na kuwajengea uelewa juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. 


Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Magu Bi. Lilian Mgonja  aliwakumbusha vijana  umuhimu wa lishe bora, na kubainisha  kuwa lishe bora na afya njema ndiyo msingi wa nguvu kazi ya taifa.



Post a Comment

Previous Post Next Post