NBAA YAWAPA MAFUNZO WANAOJIANDAA KUFANYA MTIHANI KUFANYA MTIHANI

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu akizungumza na watahiniwa  wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972 ambapo kilele chake ninatarajiwa kufanyika Novemba 28, 2022.



Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA) imewapiga msasa watahiniwa wanaojiandaa kufanya mitiahani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972.

Aliyasema hayo wakati ufunguzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu alisema; wamekua na kikao cha wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi katika ngazi mbalimbali ikiwa na lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali za mitihani hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa sana kwa watahiniwa wa Bodi.
 
Hivyo, yapo masomo ambayo yana changamoto Sana  na kiwango cha ufaulu umekuwa mdogo, tumewaletea walimu wa masomo hayo kutoka vyuo na Taasisi mbalimbali ili waweze kuwapatia uzoefu wao na kuwapa mbinu za kujiandaa na mitihani ya Bodi.

"Tumewasisitiza wasijiandae kiholelaholela bali waweke muda wa kutosha katika kujifunza kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya watahiniwa wa vyuo na watahiniwa wa mitihani ya Bodi " alisema Temu

lengo kubwa la NBAA  ni kuona wanapandisha kiwango cha ufaulu kwa mitihani pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na ukaguzi.

Kwa upande wake, Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo alisema Bodi hiyo imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mtahiniwa anafanya mitihani ya Bodi na kuhakiksiha wanaondoa changamoto zote.


Post a Comment

Previous Post Next Post