WADAU WATAKIWA KUWEKA JITIHADA ZA MAKUSUDI KUSAIDIA WABUNIFU WANAOTUMIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Picha zote na Yusuph Digossi- Sauti za Mtaa Blog 




Tanzania Ikiwa inaelekea kupiga hatua ya uchumi wa nne wa viwanda serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hawana  budi kuhakikisha  wanaongeza jitihada za makusudi ili kusaidia  wabunifu wanaotumia sayansi na teknolojia wanakuwa   wengi katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo ili kusaidia kufikia adha ya uchumi wa maendeleo endelevu.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa utafiti,sera na Mipango kutoka Mamlaka mitaji ,masoko na dhamana Alfred Mkombo  katika Warsha ya ubunifu na utafiti yenye lengo la kuangalia namna ya kusaidia biashara ndogo za Kati na kubwa kuziwezesha kupata mitaji ya masko ndani na nje ya nchi na ili iweze kuendelea lazima kuwe na ubunifu zaidi hasa vijana


Hata hivyo tupo katika mchakato  wa kushirikiana na UNDP utakotuwezesha kupata fedha kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo majukwaa,mitandao itakayosaidia kutengeneza Mpango mkakati ya kuwawezesha vijana wabunifu wanaojituma kufanya tafiti kwa kubuni namna ya kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu na kusaidia kujua tunatoka wapi na tunaenda wapi.

Kwa upande wake Promise Mwakale kutoka tume ya Sayansi na Teknolojia amesema kuwa tume hiyo imeendelea kuwasapoti wabunifu mbalimbali nchini kwa kutoa ruzuku ili kuendeleza hamasa ya vijana kuwa wabunifu zaidi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia .




Naye  Daniela kwayu Mkurugenzi wa kampuni ya iliyojikita katika kilimo Green eka ambapo wao wamekuwa waniwasaidia wakulima fedha za kuendesha shughuli zao kupata masoko 


 Meneja Mradi Ufunguo Joseph Manirakiza amesema Warsha hiyo ya wabunifu iliyofanyika ni mwendelezo wa wiki ya maonyesho ya wabunifu itakayoanza mei 16 mwaka huu Jijini Dodoma. 

Post a Comment

Previous Post Next Post