WATUMISHI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WATAKIWA KUONGEZA BIDII NA USHIRIKIANO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wafanye kazi kwa bidii huku akisisitiza  kuwa yeye kama kiongozi wao ataendelea kuwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


Ameyasema hayo leo jijini Dodoma mara baada ya kuwatembelea watumishi hao katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizoko katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kuwahakikishia kuendelea kuwapa  ushirikiano mkubwa ili waweze kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Post a Comment

Previous Post Next Post