COSTECH YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI KWA WANAWAKE NCHINI


Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano COSTECH 

Dar-es-salaam.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), inaendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ilikuwasaidia wanawake wote nchini hususani waishio vijijini kuondokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo matumizi ya nishati mbadala.

Akizungumza hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa  Sayansi na Teknolojia( COSTECH), Dk.Philibert Luhunga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake (International Women’s Day) iliyoazimishwa Jumatano ya tarehe 9 Machi, 2022 katika Ukumbi  Mkubwa wa Mikutano uliopo Jengo la COSTECH, Jijini Dar es salaam. 


Dkt. Luhunga ameongeza kuwa Tume inaendelea kufadhili miradi mbalimbali pamoja na kuwapa elimu wanawake wanaonesha jitihada za ubunifu kwa kutatua changamoto zinazoathiri wanawake kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Wako wanawake ambao wamekuwa wakifanya tafiti za nishati na mazingira ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika kuondokana na athari za tabianchi, hao ndio hasa ambao tunawapa kipaumbele," alisema.


Sherehe hizo zimehitimishwa kupitia Mdahalo uliojikita kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia-nchi uliobeba kauli mbiu ya “Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu.



Post a Comment

Previous Post Next Post