BENK YA TCB YATIKISA,YAJA NA JAMBO HILI KUBWA.





Benki ya Biashara Tanzania (TCB) leo Novemba 13,2024 imezindua bidhaa ya LIPA POPOTE, suluhisho la malipo lililobuniwa ili kurahisisha miamala kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) na wamiliki wa biashara.

Bidhaa hii mpya inawawezesha wateja wa Benki ya TCB kupokea malipo moja kwa moja kwenye akaunti zao za benki kupitia namba moja ya mfanyabiashara iitwayo LIPA POPOTE.

Zaidi ya hayo, wenye akaunti katika Benki ya TCB wataweza kulipia bidhaa na huduma kwa urahisi wakitumia namba maalum ya muuzaji (Till Number),hivyo kufanya miamala iwe rahisi zaidi kuliko hapo awali.


LIPA POPOTE imebuniwa kushughulikia hitaji la malipo ya kifedha linaloongezeka kwa kasi nchini miongoni mwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa.

Suluhisho hili linalenga kurahisisha mchakato ya malipo kwa wamiliki wa biashara, kuwawezesha kupokea malipo papo hapo na kwa usalama.

Bila kuhitaji gharama za usajili, huduma hii inapatikana kirahisi, ikiongeza wigo wa ujumuishi wa kifedha kwa kuondoa vizuizi vya miamala ya kidijitali kwa biashara mbalimbali kote nchini.

"Kwa kuzindua suluhisho la kidijitali la malipo kama vile LIPA POPOTE, tunaboresha kikamilifu malengo ya Tanzania ya kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wafanyabiashara, watu binafsi na jamii ambazo hazijafikiwa bado.




"Njia hii ya malipo inatarajiwa kubadilisha namna biashara ndogo zinavyofanya kazi, na kurahisisha miamala ya kifedha," alifafanua Bi. Lilian Mtali, Mkurugenzi wa Biashara kwa Wateja Wadogo na wa Kati,TCB.

"Tunashuhudia mageuzi ya kidijitali yanayoendelea kuboresha uchumi wetu kila kukicha, TCB inalenga kuwa mstari wa mbele katika kutoa masuluhisho ya kibenki yenye ubunifu na kuchochea ujumuishi wa kifedha kwa wote,"ameongeza Adam Mihayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post