WAKAZI Wa Mbweni Malindi wamepanda miti 2000 Kusherehekea siku miaka 62 ya uhuru kwa kupanda miti pembezoni mwa barabara ya Baraka na Flamingo kwa Kushirikiana na JKT Mbweni
Akizungumzia miaka 62 Katika tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo Clement Mshana ametoa rai kwa watanzania kujenga tabia ya kufanyakazi za kujitolea kama njia ya Kuunga mkono jitihada za serikali kutunza mazingira na kutengeneza usalama wa kizazi kijacho na viumbe au mimea
Naye Diwani wa Kata ya Mbweni Rich Mtambakike amesema Mbweni ni eneo muhimu kuwekeza miti ya kimvuli na matunda kutokana na upekee uliopo kwenye Makazi na fukwe za Kisasa, kitu ambacho kitavutia kata zingine kuhamasika kupanda miti mingi zaidi ili kutunza ikolojia iliyopo nchini
Balozi wa mazingira Moses Mwakibolwa amesema wananchi wajenge tabia ya kushiriki Katika shughuli za kijamii kama njia ya kujenga uzalendo kwa Taifa, na ameongeza kuwa wamiliki wa Mifugo kama mbuzi na ng'ombe kuacha kuchunga hivyo ili kuilinda miti inayopandwa
"Miti inaaandaliwa kwa Gharama kubwa, hivyo wananchi washiriki kikamilifu kuilinda kwa pamoja na kufukuza Mifugo kwa pamoja ili kufanikisha malengo kitaifa" alisema Mwakibolwa