Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan asherehekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.  Samia Suluhu Hassan ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo saba vya kulelea watoto yatima kama sehemu ya kusherehekea kumbukumbuku ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 63.

Rais Samia ambaye hayupo nchini amewakilishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ambaye amekabidhi vitu hivyo na kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi.


Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  ametoa wito kwa viongozi wa dini kumuombea Rais Samia ili aendelee kuliongoza Taifa kwa mafanikio ambayo yameonekana kipindi hiki cha uongozi wake ikiwemo uboreshwaji wa huduma za Kijamii

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo cha Msimbazi ‘Sister’ Stella Exavel amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa sadaka hiyo huku akibainisha kuwa wataendelea kumuombea mema na aendelee kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.


Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na pempasi za watoto, unga, sabuni, sukari, maziwa,mafuta kwa vituo vya Children home Msimbazi, Mburahati, Tua ngoma, Mbagala, Mbweni, Mwasonga na Sinza ambavyo vyote vipo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post