DKT. MPANGO MGENI RASMI UZINDUZI WA MKAKATI WA KIDUNIA KUTOKOMEZA UKIMWI KWA WATOTO IFIKAPO MWAKA 2030



Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa sekta ya Afya imeendelea kutekeleza aſuambalimbali za kumaliza janga la UKIMWI kama ilivyo malengo ya kidunia ilikapo mwaka 2030.

Tanzania imekua katika mapambano dhidi ya UKIMWI kwa zaidi ya miaka 30 na kumekuwa namafanikio makubwa katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza maambukizi ya VVUkwa watoto.Kutokana na hilo, Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa hafla ya uzinduzi wa mkakatimpya wa kidunia wa kumaliza UKIMWI kwa watoto ifikapo mwaka 2030 kwa Kanda ya Afrika.

Uzinduzi wa mkakati huu mpya, ulianza mnamo tarehe 1 Agosti, 2022, mjini Montreal Canada,ambapo ulizinduliwa rasmi ngazi ya kidunia.

Sababu kuu ya dunia kuja na mkakati mahsusi kwa ajili ya watoto ni pamoja na kutokuwepokwa uwiano chanya katika kupata huduma baina ya watoto na watu wazima unaoendelea kukuazaidi siyo tu katika upatikanaji wa huduma hizi, bali pia katika ubora wake ulimwenguni kote.

Nchi zinazotekeleza mkakati huu kwa Kanda ya Afrika ni pamoja na mwenyeji Tanzania,Cameroon, Code D'Ivore, DRC- Congo, Nigeria, Uganda, Zambia, Angola, Zimbabwe, Kenya,Afrika Kusini na Msumbiji. 

Nchi hizi, zitahudhuria uzinduzi huu Jijini Dar es Salaam, katikaUkumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 31 Januari,2023 haditarehe 1 Februari, 2023.Mgeni Rasmi katika Hafla ya uzinduzi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango.

Wizara ya Afya, inatoa wito kwa Wazazi/Walezi kuendelea kupeleka watoto wanaoishi namaambukizi ya VVU kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata tiba stahiki, Serikaliimejipanga kuhakikisha maambukizi ya VVU kwa watoto yanatokomezwa ifikapo mwaka 2030.

Imetolewa na:Aminiel Aligaesha MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINIWIZARA YA AFYA



Post a Comment

Previous Post Next Post