IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA UBUNGO



PICHA NA STORI VYOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO MANISPAA YA UBUNGO 

Mkuu wa Idara ya Utawala  na Utumishi Manispaa ya Ubungo Selemani Kateti  amefanya kikao na watumishi walio chini ya Idara ya Utawala na  Utumishi na kuwakumbusha utekelezaji wa majukumu yao wanapokuwa katika Ofisi zao kwa kusimamia majukumu yao na kufata kanuni, taratibu na Sheria za kazi

Kikao hicho kimefanyika Leo Agosti 10, 2022 ambapo Watumishi hao walipata nafasi ya kushiriki kutoa Mapendekezo na maoni  mbalimbali ili kuimarisha utendaji kazi 

Kateti, aliwataka watumishi hao Kila mmoja kujua nafasi yake anapokuwa katika kituo Chake Cha kazi ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma .


"Tujifunze kujiamini na mkasimamie ipasavyo watu mnao waongoza katika Vituo vyenu vya kazi" aliongeza Kateti.

Aliendelea kwa kusisitiza Kila mmoja kushiriki katika maswala ya kijamii ili kupeana  nguvu na faraja mtu anapopata changamoto na hata matukio ya furaha.

Aidha, Kateti  alisema pia  ushirikiano ni muhimu, upendo, kufata maadili ya kazi, kanuni, Sheria na taratibu za kazi ni Jambo la msingi Kwakila  mmoja wetu kulizingatia.


Katika swala la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri watendaji waliomba ushirikishwaji wa maafisa biashara ili  kufanya kazi kwa pamoja na kuomba uwepo wa kikao cha tathmini ambacho kitalenga kuboresha na kuongeza mapato ya Halmashauri.

Aidha, watumishi hao  walimpongeza mkuu wa idara hiyo kwa kusimamia vyema changamoto wanazozipata na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa uweledi.




Post a Comment

Previous Post Next Post