Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Nderingo Materu ( kushoto) pamoja na Haji Manara ( kulia) , wakisaini Mkataba wa makubaliano ya kibiashara ambapo Haji Manara atakuwa Balozi wa kampuni hiyo inayajihusisha na kutoa mikopo kwa watumishi wa serikali hafla iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dar es salaam.
Balozi wa Kampuni ya Bayport Haji Manara akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa Kibiashara na na kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika leo Julai 27, 2022 Jijini Dar es Salaam
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Taasisi ya kifedha ya Bayport akizungumza kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa Ubalozi na Haji Manara katika hafla iliyofanyika leo Julai 27, 2022 Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI
*****************************************
Afisa Habari wa Yanga Haji Manara amelamba bingo baada ya kutangazwa kuwa Balozi na taasish' ya Kifedha ya Bayport Financial Services kwa lengo la kufanya kazi.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Taasisi hiyo Nderingo Materu ,wakati wa halfa fupi ya utiaji saini .
Aidha,Materu amesema kuwa wamempa mkataba huo kwa sababu anauwezo mkubwa wa kufikisha ujumbe wanaoutaka kwa wateja.
“Haji Manara ni kinara na amesimama katika vitu vingi vipya, amefanya mambo makubwa sana, hivyo tumeamua kumshirikisha katika hili kwa sababu tunaamini atakuwa Balozi mzuri kwetu kwa kusaidia kufikisha ujumbe wa Taasisi yetu kwa wateja wetu,” amesema Materu.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache kupita baada ya Manara kufungiwa miaka miwili na faini ya milioni 20 na Kamati ya maadili ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) kwa kosa la kumtolea maneno ya kuudhi rais wa Tff,Warace Karia.
Sanjari na hayo,Materu amesema ndani ya miaka 16 wamefanya mambo makubwa, kwamba kwa sasa wanatoa mikopo kwa urahisi kwa watumishi wa umma kwa njia ya kidigitali.
Amesema kuwa mtumishi wa umma anaweza kupata mkopo ndani ya masaa 24 kwa kupiga simu tu jambo ambalo linasaidia kuokoa muda kwani mteja halazimiki kufika ofisini wala kujaza fomu.
Kwa upande Manara ameshukuru kwa kupatiwa Ubalozi huo ambapo ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Taasisi hiyo ili kuhakikisha inafikia malengo yake.
“Niheshima kwangu na familia yangu, ni heshima kwa Bayport, kwa Taasisi yangu ya Yanga na Tasnia ya Mpira wa Miguu ambayo nimeitumikia kwa muda mrefu,”
“Naadi mimi sina jambo dogo, nitafanya kazi kwa ukubwa, nawaahidi nitafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha mkataba huu, nitafikisha ujumbe kwa ukubwa,”.
Manara ameeleza kuwa Bayport Financial Services ni taasisi inayofanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inayoifanya ya kurahishia wateja upatikanaji wa mikopo na kwa masharti nafuu.
Tags:
BIASHARA