BENKI YA KCB YAWAPIGA MSASA WALIMU WANAOFUNDISHA VYUO VYA VETA NCHINI



Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni kutoka benki ya KCB,Pascal Machangu akizungumza  wakati wa  kuzindua mafunzo ya siku nne kwa ajili ya walimu wanaofundisha vyuo vya veta nchini yenye lengo la kuwajengea ujuzi,Mafunzo hayo yameandaliwa na Benki ya KCB kupitia pogram yake ya tujiajiri, Semina imefanyika Katika Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 27, 2022.


Baadhi ya wafanyakazi wa KCB wakifuatilia  uzinduzi wa mafunzo ya siku nne kwa ajili ya walimu wanaofundisha vyuo vya veta nchini yenye lengo la kuwajengea ujuzi,Mafunzo hayo yameandaliwa na Benki ya KCB kupitia pogram yake ya tujiajiri, Semina imefanyika Katika Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 27, 2022.
Baadhi Wakufunzi wanaofundisha vyuo vya veta  wakifuatilia  uzinduzi  wa mafunzo ya siku nne kwa ajili ya walimu wanaofundisha vyuo vya veta nchini yenye lengo la kuwajengea ujuzi,Mafunzo hayo yameandaliwa na Benki ya KCB kupitia pogram yake ya tujiajiri, Semina imefanyika Katika Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 27, 2022.

PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI

*******************************************

Na Maandishi wetu

Dar es Salaam


VIJANA nchini Tanzania wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zikiwemo za kielimu ili kujipatia ujuzi utakao wasaidia kuajiriwa na kujiajiri ili kujikwamua kiuchumi huku ikielezwa kuwa kufanya hivo wataondokana na tatizo la kusubiri ajira 

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni kutoka benki ya KCB,Pascal Machangu wakati kuzindua mafunzo ya siku nne kwa ajili ya walimu wanaofundisha vyuo vya veta nchini yenye lengo la kuwajengea ujuzi,Mafunzo hayo yameandaliwa na Benki ya KCB kupitia pogram yake ya tujiajiri.

Machangu amesema wapo baadhi ya vijana wamekuwa wakiamini maombi pekee yake bila kufanya kazi jambo linalowarudisha nyuma huku akiwahimizi kutumia fursa mbalimbali zinavyojitokeza.

Ameongeza kuwa kupitia mafunzo hayo yataweza  kuwasaidia vijana zaidi ya 200 kupata ajira huku  wengine 200 watasaidiwa kupata mitaji ya moja kwa moja.

Machangu amesema katika kufanikisha pogram hiyo imetengwa zaidi ya bilioni 1 kufanikisha ,huku akiwataka vijana wote nchini ambao wameshindwa kuendelea na shule kujitokeza kwenda KCB bank ili waweze kupatiwa fursa.

Kwa upande wake Meneja wa mradi wa 2jiajiri Betty Mruve amesema kuwa kupitia mradi huo wanatarajia kuwafikia vijana zaidi ya 900 kutoka mikoa mbalimbali yenye lengo la kuwasaidia vijana kwenda kufanya masomo darasani na nje ya darasa kwa vitendo

Naye Bahati Mwakatobe ambaye ni mwalimu wa Veta Dar es salam naye amewataka vijana nchini kuwa na nidhamu katika kazi na kujituma pamoja kuwa makini katika uchaguzi wa fani za kusema kwa kusema vijana wengi wamekuwa wakichagua fani zisizo na fursa.

Post a Comment

Previous Post Next Post