HATIMAYE MAYELE ATUA DAR USIKU HUU



Na Yusuph Digossi-Sauti za Mtaa

Baada ya tetesi za kuhusishwa na kujiunga na timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mshambuliaji wa Yanga Sc Fiston Mayele ametua Dar es Salaam usiku huu akitoa Nchini DRC Congo kwaajili ya kujiunga na kikosi cha Yanga Sc maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.

Yanga tayari imeshaanza maandalizi ya msimu mpya ambapo wameweka kambi katika Viwanja vya Avic Town Kigamboni na leo ni siku ya tatu tangu waanze mazoezi hivyo Mayele atajiunga na wenzake muda mfupi baada ya kumaliza mapumziko ya msimu uliopita.

Ujio wa mshambuliaji huyo fundi wa kucheka na nyavu ni habari njema kwa mashabki wa Yanga mara baada ya kuripotiwa kuwa nyota huyo anaweza kuondoka Jangwani kwenda kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine baada ya mafanikio aliyoyapata msimu uliopita.

Post a Comment

Previous Post Next Post