Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Tanzania (STPU) kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kuchochea migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika Kijiji cha majengo tarafa ya Manyara wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha na kusema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta wale wote waliohusika katika tukio hilo.
Kamanda Pasua amesema hayo leo Julai 25 2022 alipofika katika eneo la mashamba ya umwagiliaji ya miwaleni (scheme) ambapo amejionea uharibifu uliyofanywa na baadhi ya wafugaji katika Kijiji cha majengo tarafa ya manyara wilaya ya Monduli na kukemea vikali vitendo vya baadhi ya wafugaji wenye tabia ya kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima ambapo amesema vitendo hivyo huchochea migogoro na wakulima, Pia amewataka kufuata matumizi bora ya Ardhi ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara.
Tags:
HABARI