Tanzania imeshiriki Mkutano wa Kimataifa unaowaunganisha vijana uitwao 'Generation Connect Global Youth Summit' ulioanza Juni 2, 2022 na kuhitimishwa Juni 4, 2022, jijini Kigali, Rwanda.
Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha vijana, waliojikita katika TEHAMA, katika nyanja za ujasiriamali, uongozi, wahamasishaji wa mitandaoni, wahandisi, na watunga Sera, kujadili masuala yanayogusia mchango wa sekta ya TEHAMA katika maendeleo.
Tanzania imewakilishwa na vijana kutoka Taasisi tatu za Elimu ya Juu ambazo ni Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu- St. Joseph na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Lucy Mbogoro.
Tags:
HABARI