DKT. MPANGO MGENI RASMI KONGAMANO LA 31 LA KISAYANSI DAR ES SALAAM



Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) inatarajia kiwa mgeni rasi katika katika kongamano la 31 la kisayansi litakalofanyika kuanzia mei 17 hadi 19 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam mkurugenzi wa NIMRI, Profesa Yunus Mgaya amesema kongamano hilo linye lengo la kusambaza matokeo ya tafiti za afya zinazofanywa na watafiti wa NIMR na wadau wengine waliopo ndani na nje ya Nchi na kwamba zimebeba ujumbe usemao "Ushiriki wa Sekta Mbalimbali katika Afya ajenda ya kuimarisha Mifumo ya afya kufikia huduma ya afya Kwa Wote".

"Nafurahi kueleza kuwa mafanikio makubwa yanatokana na kuratibu makongamano kama haya,yanaleta chachu ya mwendelezo na mwaka huu (2022) tunaratibu kongamano la 31,litafanyika kwa siku ambapo atazindua rasmi tarehe 17 /05/2022 na Makamu wa rais Daktari.Philip Mpango katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere Dar see salaam". Alisema Profesa Mgaya.

Alisema kongamano hilo inasaidia kuibua na kubainisha maeneo muhimu ya afya yanayohitaji hatua za haraka za kitafiti zitakazoleta mabadiliko ya sera, miongozo, mifumo ya tiba na utendaji Kwa lengo la kuboresha afya ya jamii.

"Tuanapo zungumzia huduma ya afya kwa wote tunamaanisha wananchi wote waweze kufikiwa na huduma muhimu za afya zinazohusisha uelimishaji kuhusu afya bora, Kinga, matibabu, utunzaji wa dawa na hatimaye uboreshwaji wa maisha ya mtanzania Kwa ujumla, kongamano hili linashirikisha watalaam zaidi ya miatatu kutoka katika taasisi mbalimbali za kitaifa nchini naza kimataifa wakiwemo watafiti na watunga sera".

Aidha Prof. Mgaya aliongeza kuwa katika kongamano hilo maandiko zaidi 260 ya kisayansi yanatarajiwa kuwasilishwa kupitia mada ndogo ndogo zitakazohisu Magonjwa mbalimbali vichocheo vyake na ufanisi katika mfumo wa afya kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Magonjwa ambukizi,tiba asili, usugu wa dawa katika tiba ya magonjwa na mifumo ya udhibiti wa magonjwa.

Maeneo mengine ni afya ya mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Magonjwa yasiyoambukiza, huku eneo jingine ni changamoto za afya zitokanazo na janga la UVIKO 19, Lishe, Afya ya mama, mtoto na vijana, magonjwa yasiyopewa kipaumbele pamoja na udhibiti na usimamizi wa tafiti za Tiba.

"Jumla ya maandiko 260 ya kisayansi yanatarajiwa kuwasilishwa katika kongamano hilo kupitia mada zitakazohusu magonjwa mbalimbali na vichocheo vyake na ufanisi katika mfumo wa afya ikiwemo magonjwa ambukizi yanayoibuka na yabayojitokeza baada ya kutokomezwa, tiba asili, magonjwa yasiyoambukiza" alisema Prof Mgaya

Post a Comment

Previous Post Next Post