PAPE SAKHO AITANGULIZA SIMBA KWA MKAPA



Na Yusuph Digossi 

Dakika 45 za mchezo wa kombe la shirikisho Barani Afrika zimekamilika  katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mnyama Simba kutangulia kwa Bao 1mbele ya mgeni Rs Berkane.

Ni Pape Osman Sakho aliyewatanguliza Simba mnamo dakika ya 44 baada ya kuwachambua kama karanga walinzi wa Berkane na kupiga shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango

Simba SC wana kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo uliopita ugenini kwa 2-0 kutoka kwa Rs Berkane , leo wanataka kulipa kisasi na kupata alamu 3 muhimu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuongoza kundi na kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo yenye heshima kubwa Barani Afrika. 

Simba walianza  mchezo kwa kasi kwa kupeleka mashambulizi ya hatari katika lango la wapinzani licha ya Berkane kuonekana kuwa wagumu lakini juhudi zao zilizaa matunda na wanakwenda mapumziko wakiwa na bao moja .

Kocha Pablo amefanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chache ikiwa ni tafsiri ya kutaka kushambulia zaidi na kupata mabao mengi,  Kibu Denis amerejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kukosekana kwa kipindi kirefu kutokana na kuwa majeruhi,  pia kiungo Bwalya.

Post a Comment

Previous Post Next Post