Picha na mtandao wa Simba |
Na Yussuph Digossi- Sauti za Mtaa
Dakika 45 za mchezo wa ligi kuu ya NBC kati wenyeji Simba dhidi ya Dodoma zimekamilika katika uwanja wa Benjamini Mkapa na hakuna mbabe si mgeni wala mwenyeji aliyeona lango la mwenzake.
Kama ilivyo kawaida ya falsafa yao Simba walianza mchezo kwa kasi na kupiga pasi fupifupi kuelekea lango la Dodoma Jijini na kutengeneza nafasi kadhaa lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji ikiongozwa na beki kisiki George Amani Wawa iliwanyima nafasi ya kuandika bao la kwanza .
Kwa upande wa Dodoma Jiji muda mwingi walionekana kucheza kwenye eneo lao la ulinzi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza kupitia mshambuliaji Seif Karihe ambae alikuwa chini ya ulinzi mkali wa safu ya ulinzi ya Simba.
Nahodha John Rafael Bocco alishindwa kuendelea na mchezo mnamo dakika ya 28 na nafasi yake kuchukuliwa na Meddie Kagere .
Simba inawakosa walinzi wake Shomary Kapombe na Henock Inonga kutokana na kuwa majeruhi.
Je Simba itafanikiwa kufungua safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji na kuandika bao ? endelea kusalia na Sauti za Mtaa Blog kwa taarifa zaidi.