Katika kuhakikisha jamii ya watanzania inaendelea kupata habari za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu WAHARIRI wa vyombo vya habari mbalimbali wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) lengo likiwa ni kuongeza tija eneo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na (STU) nchini.
Ahadi hiyo wameitoa jijini Dar es salaam wakati wa warsha ya mafunzo ya kutazamia nafasi ya wahariri katika uzalishaji na usambazaji wa habari za sayansi, teknolojia na ubunifu iliyofanyika leo tarehe 31 Machi 2022 iliyoandaliwa na COSTECH kupitia kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) ili kutengeneza mkakati madhubuti utakaosaidia kuzalisha na kusambaza makala nyingi zaidi za mafanikio ya miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ili wananchi wafahamu kazi kubwa inayofanywa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Bugwesa Katale akifungua mafunzo hayo alisema COSTECH ni Taasisi ya Umma na moja ya jukumu lake kubwa ni kuishauri Serikali pamoja na kuratibu na kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu hapa nchini, kwa kuandaa agenda za utafiti za Utafiti na unadaaji wa nyaraka mbalimbali za namna ya kuongoza tafiti na bunifu zinaweza kuendeshwa hapa nchini.
“Leo tuko hapa katika kuhakikisha tunaendeleza jukumu la kusambaza habari za sayansi, teknolojia na ubinifu. Vilevile Tume ina Kurugenzi nne ambazo ni Kurugenzi ya Uendelezaji na Usimamizi wa Tafiti, Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa, Kurugenzi ya Huduma za Taasisi na Kurugenzi ya Uhawalishaji wa Teknolojia na zinafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunapata matokeo ” alisema.
Dkt. Bugwesa aliongeza pia Tume ina vitengo vinavyosaidia utekelezaji wa kazi zake na mojawapo ni Mfuko wa Taifa wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) kazi yake kubwa ni kufadhili miradi ya utafiti na ubunifu nchini.
Tags:
TEKNOLOJIA