Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Februari 17, 2025, amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yameambatana na kliniki za huduma katika mikoa saba nchini, zikilenga kutoa elimu kwa wadau muhimu wa masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Kaulimbiu ya maadhimisho ni "Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu – Athari chanya, ubunifu na huduma."