Katika kuwafikia baadhi ya waumini wa kiislamu wenye uhitaji maalumu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Taasisi ya LALJI FOUNDATION chini ya mwenyekiti wake Imtiaz Lalji imetoa futari kwa wakazi wa magomeni jijini Dar Es Salaam ikiwa ni mara ya pili kutekeleza zoezi hilo lengo likiwa ni kuwashika mkono waislamu wasioweza kumudu gharama za futari katika mwezi huu.
Akizungumza wakati wa kugawa futari hizo Ndugu Imtiaz Lalji amesema kuwa wataendelea kuwashika mkono wale wote wanaofunga na kushindwa kumudu gharama za futari hususani katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani .
Kwa upande wake sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar amesema kuwa zoezi hilo ni moja ya maelekezo ya Mtume Muhammad (S.W.A) ambapo ameipongeza taasisi ya LALJI FOUNDATION foundation kwa kutekeleza zoezi hilo huku akiwataka wadau wengine nchini kuunga mkono juhudi hizo katika kuwafutirisha wale wasio weza kumudu gharama
Nao baadhi ya wanufaika wa msaada huo akiwemo maalim Baraka Mwinyimkuu pamoja na Aisha Abubakar wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapa futari huku wakiaombea heri ili waendelee kutoa msaada huo kwa wananchi wengi zaidi.