Wadau wa habari watolewa hofu muswada wa sheria ya huduma za habari kusomwa bungeni



Na Yusuph Digossi, Dar es Salaam 

 Mwenyekiti wa Jukwaa la wahari Tanzania TEF Deodatus Balile amewataka wadau wa habari nchini kuwa na subira wakati muswada wa sheria ya huduma za habari ukisubiriwa kuingizwa na kujadili bungeni katika vikao vya bunge la 12 vinavyoendelea jijini Dodoma. 

Balile ameyasema hayo Leo Ijumaa Feb 3, 2022 alipokua akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa umoja wa taifa na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu ushirikiano wa UN na vyombo vya habari Tanzania katika maeneo mbalimbali.


" Nina taarifa za uhakika kwamba mpaka jana jioni kulikua na kila dalili kwamba mswada utaingizwa bungeni na nimeambiwa tusiwe na wasiwasi mswada utaingia bungeni na kitakachobadilika nadhani mswada hautoonekana kwa njia ya kawaida" amesema Balile.

Balile amesema wadau wawe na subira wanaendelea kuwasiliana na mamlaka , serikali na watunga sera ili kuona jinsi gani sheria itakavyokwenda huku akisisitiza kua kuna kila dalili ya sheria hiyo kuingia bungeni.

Kwa upande wake Zlatan Milisic, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania ameshauri wahariri wa vyombo vya habari kuwa karibu na wananchi ili kusaidia kushiriki katika vita ya ukatili kwa wanawake, watoto pamoja na mila potofu.


Post a Comment

Previous Post Next Post