JUMUIYA YA SHIA TANZANIA YAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUMUENZI IMAM HUSSEIN a.s




Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'asharia Tanzania T.I.C Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge Amesema Imam Hussein a.s alikufa kwaajili ya Kusimamisha Dini na Uislamu Asili wa babu yake Mtume Muhammad [s.a.w.w] na Sisi ni lazima tumuenzi Imam Hussein [a.s] kwa kusimamisha Dini ya kiislamu maana Dini ya kiislamu inalingania Mshikamano, Upendo, Huruma,Umoja baina ya waislam na okwasiokuwa Waislamu na Kupinga Dhulma, Fedheha, Unyanyasaji, Mauwaji. Kisha alisema Imam Hussein [a.s] alipigania Amani nasisi tunaahidi Kulinda Amani ya Dunia na Hasa Nchi yetu ya Tanzania.

Sheikh Jalala Ameyasema hayo katika Matembezi ya Kumbukizi ya Kumuenzi Mjukuu wa Mtume Muhammad [s.a.w.w] Imam Hussein [a.s] aliyeuwawa Karbalaa kwa Dhulma na Fedheha. 

Matembezi yaliyoanzia Ilala Boma - Uwanja wa Pipo Kigogo Post



Post a Comment

Previous Post Next Post