MCHAKATO WA MABADILIKO YA SHERIA UNAHUSISHA WANAHABARI WENYEWE
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile amesema kuwa mchakato wa mabadiliko ya Sheria za habari nchini Tanzania unashirikisha wanahabari wenyewe kupitia vikao na mikutano ya mara kwa mara ambapo wanahabari hufanunuliwa vifungu vya sheria vinavyopendekezwa kufanyiwa mabadiliko.
Amesema TEF imekuwa ikifanya mikutano na Wahariri , waandishi pamoja waandishi wa habari za mitandao kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwafafanulia kuhusu vifungu vya sheria.
Balile ameyasema hayo ) wakati akizungumza katika Kipindi cha Mezani kinachorushwa na Kituo cha Redio cha EFM, jijini Dar es Salaam.
“Vikao hivi tumevifanya mara kwa mara na waandishi wanaelewa, na hatua iliyopo sasa ni kwenda kwenye mjadala ulioitishwa na Wizara ya Habari, Mawasilia na Teknolojia ya Habari tarehe 11 – 12 Agosti mwaka huu kwa ajili ya kupitia vifungu vinavyolalamiukiwa,” amesema.
Balile ameongeza kuwa haki ya uhai haipo kwenye mikono ya mwanadamu yeyote lakini haki ya habari inapangwa na wanadamu namna ya kuitumia.
“Tunataka sheria hizi za habari zitupe mwongozo wa msingi. Baada ya haki ya uhahi, kinachofuata ni haki ya kupata habari,” amesema Balile wakati akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari nchini.
“Kuna mfumo wa kwanza ni self regulation (kujitathmini), mfumo wa pili ni serikali ‘kushika’ vyombo vya habari kama ilivyo sasa na mfumo wa tatu ni co-regulation ambapo serikali na wadau wa habari wanakuwa na chombo ambacho kinawaunganisha.
Amesema, TEF kwa kushirikiana na wadau wa habari nchini, wanapendelea mfumo wa tatu ambao unatoa fursa kwa pande zote mbili (wadau na serikali) kuwa na sehemu ya kukutana pale kunapokuwa na malalamiko.
Tags:
HABARI