MFUMO WA KIDIGITALI KUTUMIKA KUKUSANYA TAARIFA ZA WATANZANIA



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anna Makinda amesema mfumo wa kidigitali ndio utakaotumika kukusanya taarifa za watanzania tofauti na mfumo wa kianalogia uliokuwa ukitumika kukusanya taarifa mwaka 1967 lilipofanyika zoezi hilo kwa awamu ya kwanza. 

Kamisaa Makinda ameyasema hayo katika Mkutano wa viongozi wa dini, Wakuu wa wilaya,  Wakurugenzi pamoja na makatibu tawala kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 uliofanyika jijini Tanga ambapo Kamisaa Makinda amesema wanatarajia katika zoezi hilo kila mtanzania atahesabiwa kwa maslahi ya Taifa. 

Kamisaa Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika mkutano huo amewaagiza viongozi wa dini na kimila kwenda kutumia majukwaa yao na nyumba za ibada kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi hilo la kitaifa  itakapofika  Aguost 23, 2022.


"Lengo la serikali katika Sensa ya mwaka huu  ni kuhakikisha tunapata takwimu sahihi kusudi iweze kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kulingana na uhitaji mazingira yaliyopo hivyo ni  takwimu tulizonazo hatutaki ziishie kwenye vitabu tunataka zishuke  hadi kwa wananchi wa hali ya chini ili tuweze kujua pia uchumi wetu umekuwa kwa kiasi ganu" alisema Makinda.

Aidha Makinda alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha inapata takwimu za wafanyabiashara wadogowadogo maarufu Kama wamachinga ili kuendelea kuweka mazingira wezeshi ambapo limeandaliwa dodoso rasmi kwaajili yao ili kuweza kuwatambua kwa idadi.


"Katika Sensa  hii ya mwaka 2022 kutakuwa na dodoso maalumu la wamachinga ili kuweza kuwatambua  watakuwa na  kadi za kudumu hivyo ni kitu ambacho kitasaidia  sana pamoja na  serikali yetu" alisema Makinda.

" Kazi ambayo ipo kwetu sisi wote  ni kuelimisha na kuhamasisha  lakini bila viongozi wa dini na kimila hatuwezi  kufanya kazi peke yetu  hivyo viongozi wa dini tunawaona  Kama ni watu  ambao wanasikilizwa  na jamii tungekuwa tukiwatumia kila mara  na tunaamini watatusaidia " aliongeza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amesema zoezi hilo lina manufaa makubwa kwa Taifa na kutaka jamii kujitokeza na kuhesabiwa. 

Malima  alisema kuwa wamejipanga pamoja na kamati za mkoa wilaya na viongozi wote kuhakikisha kuwa Tanga inakuwa msatari wa mbele kufanikisha Zoezi hilo kwa ngazi ya kitaifa.

"Licha ya kuwa mkoa wa atanga no mkubwa kiutawala  lakini tunaamini kuwa tutahakikisha na tumejipanga  kuwa wa kwanza kufanikisha Zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na hii tumejipanga kufanya vikao na viongozi wa dini wa mila  pamoja na kamati  za senza katika Tanga hii Mimi nikiwa ni mkuu wa mkoa naomba mtambue kuwa nimeweka maendeleo' mbele"

" Tutahakikisha kuwa  viongozi wa dini wanafikisha ujumbe kwa waumini na Wananchi wote kwa ujumla nikiamini zaidi kuwa  katika kufanikisha  hili viongozi wote wa dini mnayi nafasi katika kufanikisha Zoezi hili la kitaifa" 

Aidha Malima ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga  alibainisha kuwa hatomvumilia mtu au kikundi chochote Cha watu watakaojaribu na kutaka kukwamisha kufanikisha Zoezi la Sensa ya watu na makazi badala  watakutana na mkono wa sheria.


"Pamoja na sura ya uelimishaji na uhamasishaji pale ambapo tutakuta  Kuna mtu au watu wanaoenda kinyume au kupotosha  suala hili la Sensa ya watu na makazi tutamshughulikia  kisheria ,  mimi agenda yangu nikiwa ni mkuu wa mkoa wa Tanga  ni kuhakikisha maendeleo' ya mkoa yanapatikana "

Awali akitoa taarifa ya maandalizi ya Sensa mtaalamu wa habari na mawasiliano  kutoka ofisi Taifa ya Takwimu  Said Ameir alisema kuwa Sensa ya mwaka 2022 ambayo ni ya sita hapa nchini kufanyika  itafanyika  tofauti na awamu zote ambapo  karani  atarekodi taatifa za kila kaya kupitia simu janja  ambapo takwimu zitakuwa  zinapatikana  katika kila kitongoji kwa kila eneo husika.

" Hii itatusaidia  kukusanya  taarifa za takwimu  na kujua ni wapi panahitaji huduma gani Jambo kubwa ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatoa taatifa sahihi kwa makarani, kabla ya Sensa karani atatembelea  eneo lake la kuhesabia kwa lengo la kujua  na kutambua  ni huduma gani za kijamii  zinapatikana  kwa kushirikiana na viongozi wa eneo husika" alisema Am

Viongozi wa dini wameahidi kutumia majukwaa yao kuhamasisha jamii dhidi ya zoezi hilo kwa muhimu kwa maendeleo ya Taifa. 

Zoezi hilo la sensa ya watu na makazi linatarajiwa kufanyika agosti 23 mwaka huu na linafanyika ikiwa ni awamu ya sita tokea zoezi la sensa kufanyika mwaka 1967 kwa mara ya kwanza. 




Post a Comment

Previous Post Next Post