BENKI YA KCB YATOA WITO KWA WADAU KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUSAIDIA WATU WENYE CHANGAMOTO YA UGONJWA WA SARATANI

Katika kuadhimisha siku ya mashujaa wa Saratani Duniani,  Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB akipokea cheti kutoka kwa Mganga Mkuu wa Serikali,  Dkt. Aifello Sichalwe , kwa kutambua mchango wa Benki hiyo kusaidia mashujaa na wagonjwa ambao wanaendelea kupigana na ugonjwa huo,  maadhimisho yalifanyika jana Jumapili Juni 5, 2022 Katika Hospitali ya Ocean Road,  Jijini Dar es salaam


Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB,  Christina Manyenye akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa wa Saratani ambayo huadhimishwa kila Ijumaa ya kwanza ya Mwezi 6, mwaka huu yamefanyika katika Hospitali ya Ocen Road Jijini Dar es salaam

Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB, Christina Manyenye ( wa kwanza kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Shujaa Cancer Foundation ( wa pili kushoto), Mganga Mkuu wa serikali Dkt. Aifello Sichwale, Mgeni rasmi ( wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road,  Dkt. Julius Mwaiselage ( wa pili kulia) wakiwa katika maadhimisho ya siku ya mashujaa wa Saratani yaliyofanyika katika Taasisi ya Ocean Road leo Jumapili Juni 5, 2022 
Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB,  Christina Manyenye akifurahia jambo na baadhi ya mashujaa wa Saratani wakati wa Maadhimisho ya siku ya mashujaa wa Saratani katika Viwanja vya Taasisi ya Ocean Road,  Leo Jumapili Juni 6, 2022 Jijini Dar es salaam 

PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG 

*******************************************

NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG 


Katika kuhakikisha ugonjwa wa  kansa unafutika pale panapowezekana Benki ya KCB imeiomba jamii kuwasaidia wale ambao wamekumbwa na wanaopambana na ugonjwa huo kwa kutoa misaada mbalimbali. 

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa masoko wa Benki ya KCB, Christina Manyenye wakati wa Maadhimisho ya siku ya mashujaa wa Saratani ambayo huadhimishwa kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa sita ambapo kwa mwaka huu yameadhimishwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.


Siku hii imebeba ujumbe mzito uliojikita katika kutoa elimu kuwa  saratani inatibika tukiweza kuiwahi mapema kabisa ikiwa katika hatua za awali, na pia kuwa na saratani siyo kikomo cha kutimiza malengo yako. 

Katika maadhimisho haya Benki ya KCB imeshiriki kama mdhamini na mdau muhimu ambapo wameendelea kutoa misaada ili kusaidia watu wanaopambana na ugonjwa wa Saratani. 


Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho hayo Mkuu huyo wa masoko amesema wao kama Benki ya KCB  wameendelea kutoa misaada kwa watu wenye kansa katika hospitali mbalimbali ikiwemo Ocean Road kwa kutoa vifaa tiba lakini pia ukarabati wa majengo.


Amesema Mbali na kansa, Benki ya KCB  imetoa misaada mingi kwa hospitali mbalimbali hapa Tanzania hasa kwa upande wa wakina mama (wodi ya wazazi) na watoto.

Aidha amesema ni jukumu la kila mtu kumuwezesha kijana mwenye kansa hasa kwa kumpa elimu na kumpitisha katika ujasiriamali;

"Benki ya KCB tunawasaidia wanawake na vijana ili waweze kuzintunza familia zao endapo watakutana na magonjwa Kama haya ya kansa au changamoto nyingine za kijamii"

"Kansa ni ugonjwa na kushughulika ili kuiondoa hii kansa ni kitu ambacho unaweza ukakiangalia kwa namna moja au kwa upana zaidi, kwa sisi KCB tumeona kwamba watu wanahitaji kuwezeshwa hivyo tunawezesha vijana kwa kuwapeleka wakasome mfano kwenye chuo cha ufundi (VETA) na kuwapitisha katika ujasiriamali na wengine kuanzisha biashara zao wenyewe lakini pia kuwapa mikopo nafuu" 

Aidha Manyeye amesema Changamoto kubwa ni watu  kuogopa kupima kansa,  lakini ni vyema ukiwahi kupima na kapata matibabu mapema.

Amesema Katika vijana ambao wamewasaidia wa mwaka 2019 yupo mmoja  ambaye alikutwa na kansa hivyo wao kama Benki ya KCB wanaangalia namna ya kumsaidia kijana huyo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa serikali, Dkt. Aifello Sichwale amesema nia ya siku hii ni kusherehekea mafaniko ya mashujaa waliowahi kuugua saratani lakini pia kuwapa moyo wale waliogundulika na saratani hivi karibu lakini pia kwa wanaoendelea na matibabu.


Dkt. sichwale amesema waathirika ni wengu wapo walioathirika moja kwa moja lakini pia wasioathirika moja kwa moja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage ameishukuru serikali kupitia kitengo cha MSD kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kemia ambapo kwa sasa zinapatikana kwa takribani 95%-98% 

Kwa upande wake mmoja wa shujaa wa kansa Duniani amesema matibabu yanapatikana na muhimu watu wajitokeze mapema, wake kwa waume wapate matibabu sahihi ambapo kwa Ocean Road yanapatikana

Mapema asubuhi maadhimisho hayo yaliambatana na matembezi ya amani ya kilometa 6, ambapo viongozi,  mashujaa wa kansa na wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo walipata fursa ya kutembea kwa pamoja kama ishara ya amani na upendo pamoja na kuhamasisha watu kufanya mazoezi ili kujenga afya zao na kujikinga na magonjwa mbalimbali 

Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB, Christina Manyenye akiwa katika matembezi ya amani wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mashujaa wa Kansa. ( Picha na Yusuph Digossi) 



Onyesha Upendo, epuka Unyanyapaa, Shirikiana vyema na Mashujaa wa kansa . Benki ya KCB  inawatambua  mashujaa  wa saratani na inawapongeza kwa kumaliza tiba, saratani inatibika.

Post a Comment

Previous Post Next Post