WAZIRI MKENDA ATEMBELEA TAASISI YA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU CHUO KIKUU NORTHANMPTON-UINGEREZA Na WyEST-





London Uingereza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Mei 25, 2022 ametembelea Taasisi inayojishughulisha Teknolojia na ubunifu wa mazao yatokanayo na ngozi ya Chuo Kikuu cha Northampton nchini Uingereza. 

Akiwa katika Chuo hicho Waziri Mkenda amefanya mazungumzo na uongozi 10 wa Juu wa Chuo hicho na kukubaliana kuwa na Makubaliano maalum (MoU) ya kuwezesha kuanza kubadilishana uzoefu watumishi wa Chuo hicho na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) pamoja na kuanza kutoa ufadhili (scholarship) kwa wanafunzi wa Kitanzania katika eneo hilo. 


Aidha Prof. Mkenda amefurahi kukutana na wanachuo wawili wa Kitanzania, William Lohay na Azaria Chongeri wanaosoma chuoni hapo ambao ni watumishi wa DIT kampasi ya Mwanza ambayo ni mahsusi kwa eneo la teknolojia ya mazao ya ngozi. Waziri Mkenda yuko nchini Uingereza ambapo anahudhuria kongamano la Mwaka la Kimataifa la Elimu (World Education Forum 2022). 



Post a Comment

Previous Post Next Post