Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Sensa ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu (wa kwanza upande wa kushoto) akitazama ripoti ya taarifa ya Sensa ya Watu na Makazi iliyoandaliwa mahsusi kuelekea zoezi linatorajiwa kufanyika nchini kote, Agosti 23, 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Sensa ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu akizungumza na Wawakilishi Sekta Binafsi, Wafanyabiashara na wadau wengine wa Sensa ya Watu na Makazi kuelekea zoezi hilo linalotarajaliwa kufanyika Agosti 23, 2022 nchini kote.
********************************************
Na Yusuph Digossi
Wafanyabiashara wameshauriwa kufanyia kazi wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu katika kukamilisha zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kusaidia kuweka matangazo ya nembo ya Sensa kwenye bidhaa mbalimbali ili kuhamasisha zoezi hilo nchi nzima .
Hayo yamebainishwa na MWENYEKITI wa Kamati ya Ushauri ya Sensa, Dkt. John Jingu jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wawakilishi wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara kuelekea katika zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 31 mwaka huu.
Akizungumzawakati alipokutana na Wawakilishi hao Dkt. Jingu amesema licha ya maandalizi hayo kufika asilimia 80%, kazi ya kukamilisha na kufanikisha zoezi hilo kwa asilimia zote 100% inaendelea sehemu mbalimbali nchini bila kuchoka.
"Sensa hii itakua ni sensa ya sita tangu nchi yetu ilivyoanza hivyo ni jambo kubwa ambalo linafanyika kila baada ya miaka 10 na mwaka huu tunabahati ya fursa ya kufanya sensa ya kitaifa" Amesema Jingu
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza kutoka Zanzibar ofisi ya makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Thabit Faina amesema Suala la uhamasishaji wa sensa linakwenda vizuri kwa kiasi kikubwa na sasa wamebakisha hatua ndogo ya 20%.
Pia Faina amesema Matarajio yao ni kuona wapi panahitaji huduma ya Afya, kujenga shule mpya, kuwekeza aina ya biashara mbalimbali katika maeneo tofautitofauti.
Akizungumza kwa niaba ya Sekta Binafsi, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Paul Makanza amesema kupitia zoezi hilo la Sensa, Sekta binafsi itafaidika na takwimu hizo za idadi ya watu na makazi na kuzifanyia kazi ipasavyo hususani katika Sekta ya Biashara kulingana na uhusiano wa Sekta hiyo na idadi ya watu.
Tags:
HABARI