VIONGOZI WA MASHIRIKA NA WAENDESHA MIRADI NCHINI TANZANIA WAJENGEWA UWEZO WA KUBUNI NA KUENDELEZA MIRADI BORA YENYE KULETA MANUFAA KWENYE JAMII



Na Yusuph Digossi- Sauti za Mtaa Blog

Viongozi wa mashirika na wabunifu wa miradi wametakiwa kubuni na kuendesha miradi iliyobora, inayotekelezeka ili iweze kuleta tija na manufaa katika jamii. 


Rai hiyo imetolewa na mshauri wa kimataifa kutoka shirika la CESO la nchini Canada , Bryan  Marshman wakati wa mafunzo yaliondaliwa na taasisi ya community Hands Foundation kwa kushirikiana na CESO yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo viongozi na waendesha miradi kutoka mashirika mbalimbali  yaliyofanyika katika Ofisi za Community Hands Mwenge  Jijini Dar es salaam leo Alhamisi mei 12-2022.


Marshaman amesema kuwa wabunifu wa miradi wengi wamekuwa wakibuni miradi bila kufanya utafiti wa kutosha na hatimaye miradi hiyo kukwama na kuishia njiani na kushindwa kufikia malengo ya miradi hiyo.


Bryan Marshaman akawataka wanufaika wa mafunzo hayo kuyatumia kama Nyenzo muhimu ya kubuni na kuendesha miradi iliyobora , yenye tija na inayotekelezeka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Community Hands Foundation , Paul Makoe amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwasababu wanufaika watajengewa uwezo wa kubuni miradi itakayoweza kutekelezeka na kuleta tija kwa jamii.


Amesema mafunzo hayo yaliambatana na shuguli mbalimbali kama vile ubunifu wa miradi,  uendeshaji wa miradi ya kijamii, matumizi sahihi ya fedha za miradi na mambo mengine.

Amesema mradi huo umebuniwa baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa viongozi wa mashirika  na wabunifu wa miradi kuhusu changamoto katika uendeshaji na usimamizi wa miradi.



Mafunzo hayo pia yalihudhuriwa na Taslim Madhani pamoja na Michael Dalali wawakilishi kutoka ubalozi wa Canada.

Katika hotuba yake Taslim Madhani alipongeza juhudi zinazofanyika na Shirika la Community Hands Foundation kwa kushirikiana na CESO kwa kuendesha mafunzo hayo ambayo yanalenga kuleta matokeo  chanya.






Post a Comment

Previous Post Next Post