Na Hadija Bagasha Tanga,
Jumla ya Mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar itanufaika na mradi wa USAID- Afya yangu unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Ajapaigo kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa lengo la kuboresha utoaji huduma za afya, uzazi wa mpango sambamba na kupambana na tatizo la vifo vya akina mama na watoto hapa nchini.
Akizindua mpango huo Mkoani Tanga mkuu wa mkoa Adam Malima akiwa katika kikao cha pamoja na mkurugenzi wa huduma za Afya ustawi wa jamii na Lishe kutoka ofisi ya Rais Tamisemi wawakilishi wa shirika la Ajapaigo wakurugenzi na watumishi wa Afya na wadau aliwataka kujenga ukaribu pindi mama anapokuwa mjamzito ili kuweza kuepukana na athari ambazo zimekuwa zikijitokeza ikiwemo vivyo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Mkoa wa Tanga wenye Halmashauri 11 na wilaya 8 ni miongoni mwao mikoa 11 itakayonufaika na mradi huo wa Afya ambapo wanawake kati ya 1000 wanaojifungua kwa mwaka 77 hupoteza maisha pamoja na watoto.
Kutokana na takwimu hizo Malima amemuagiza mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Jonathan Budemu kwenda kuhakikisha wanapunguza na kuondokana kabisa na vifo vya akina mama na mtoto vinavyotokea wakati wa kujifungua na ili kuwa mstari wa mbele katika kunufaika na mradi huo ambao utatekelezwa kwa jumla ya miaka mitano.
"Majanga mengi wengi wao wanakutana nayo wakati wakiwa kwenye vituo vya afya uwezo wa kuongea na mama kukaa naye karibu atakusaidieni kuelewa changamoto zote ambazo anakumbana nazo nyumbani na hii itakuwa ni njia ya kuzuia au kuondokana na vifo vya akina mama na watoto kuna njia nyingi ambazo zitahitaji nguvu kati yenu wauguzi na sisi kuhakikisha tunakabiliana na changamoto hii"alisema Malima
"Mradi huu unaanza tukiwa kwenye vifo 77 ukimalizika nataka tuwe chini ya 30 , mganga mkuu wa mkoa ninakuomba nendeni mkapambane kuishusha namba hii kutoka 77 tulipo kwa sasa lazima nyinyi muwe na uwezo wa kutafuta njia ya kuondoa tatizo hili, sisi viongozi tukilisemea lazima tufanikiwe anapokaa mtu wa Afya afikirie namna ya kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hili"aliongeza
Akizungumza Mkurugenzi wa mradi huo Dkt. Rita Noronha alisema kuwa lengo kuu ni kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango , Afya mama na mtoto pamoja na Afya ya uzazi pamoja na kubadilisha mtazamo wa walengwa kwenda kituoni kupata huduma ili kuendelea kuwasaidia na kuondokana kabisa na changamoto ya vifo vinavyojitokeza wakati wa uzazi.
Dkt Noronha alisema kuwa pamoja na kuboresha huduma za Afya ni pamoja na kutoa kinga kwa mama na mtoto kama ilivyo adhima ya serikali ambapo kupitia wizara ya afya imekuja na mpango mikakati wa kuhakikisha kuwa inatokomeza vifo vya mama na mtoto kutokana na ujauzito na wakati wa kujifungua.
Aidh alibainisha kuwa mradi wa huo ambao ulizinduliwa na waziri mkuu Kassimu Majaliwa mkoani Dodoma ni mradi wa miaka mitano ambapo utaghalimu dolla za kimarekeani Million 66.8 ukitekeleza katika mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar.
"Mradi huu ni mpya hapa nchini na lengo kubwa ni kuboresha huduma za Afya upatikanaji na huduma za uzazi wa mpango, inatekelezwa katika mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar, lengo pia ni kuisaidia wizara ya afya katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto, kubadilisha tabia za watumiaji ili waweze kuja vituoni na kupatiwa huduma na hii ni kutokana na takwimu ambazo zinatuonyesha mapungufu yakowapi , Tunategemea tutakapotwkeleza huu mradi tuweze kuinua na kuboresha afya ya mama na mtoto, alisema Dkt Noronha.
Kwa upande wake mkurugenzi wa huduma za Afya ustawi wa jamii na Lishe kutoka ofisi ya Rais Tamisemi Dkt Ntuli Kapologwe alibainisha kuwa katika kuhakikisha huduma za Afya ya mama na mtoto zinaboreshwa mpaka sasa serikali imejenga vituo vya afya 746 , hospitali za halamashauri 140 pamoja na zahanati 2500 ndani ya miaka mitano ambapo uboreshaji wa miundo mbinu hiyo unaenda sambamba na kuhakikisha inaimarisha utoaji wa huduma.
"Serikali imekuwa ikiwekeza fedha nyingi kwa upande wa afya hasa kuboresha afya ya mama na mtoto ujenzi wa miundo mbinu ya afya unaenda sambamba na utoaji huduma bora na hapa ndipo wenzetu wa Ajapaigo wanapoingia kutuunga mkono , sisi kama wasimamuzi wa mpango huu tunaamini kuwa mafanikio yatakuwa ni makubwa na utekelezaji wake ni wa mafanikio.alisema Dkt. Kapologwe.
Alisema kuwa bado takwimu za kitaifa katika vifo vya akina mama na watoto ni kubwa hivyo kuwataka wahudumu na watumishi wote wa Afya kuhamasika na kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote yanatolewa na serikali katika kupambana na changamoto hiyo huku akiwataka wananchi kuelimika na kupata huduma ili kujikinga zaidi.
"Takwimu zetu za kitaifa bado tuko vizazi hai laki 100,000 kuna vifo 556 hivyo bado hivyo vifo ni vingi sana sisi kupitia uzinduzi huu tutaweka mikakati ya kitaifa kuanzia mamlaka za serikali za mitaa wadau wanakuja sisi kama serikali kuwa kushirikiana nao tutafanikiwa kupunguza na kuondokana na vivyo vya akina mama na watoto"alisema
Dkt Kapologwe alizitaka kamati zote zinazosimamia mpango huu kuanzia ngazi za mikoa kuhakikisha zinatekeleza kwa kwa vitendo mradi huu kikamilifu ili kuendana na adhima ya serikali kuwa ushirikiano na wadau wa Afya kupunguza na kutokomeza kabisa vifo vya akina mama na watoto ambavyo vinapunguza nguvu kazi ya taifa.
Tags:
HABARI