Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam leo tarehe 25/05/2022 limefanya kikao cha mapitio ya taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi Cha robo ya tatu yaani mwezi Januari mpaka Machi 2022.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Arnatoglo kimeongozwa na Naibu Meya wa jiji la Dar es salaam Mhe.Saady Khimji na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali wakiwemo wakuu wa Idara,Watendaji wa Kata zilizopo katika Halmashauri ya jiji la Dar es salaam na wanahabari.
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bi.Tabu Shaibu amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022,Halmashauri ya jiji la Dar es salaam imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha jumla ya shilingi Bilioni 191.9 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 122.3 ni ruzuku kutoka Serikali kuu ambapo Shilingi Bilioni 98.1 ni mishahara na Shilingi Bilioni 1.8 ni matumizi mengineyo na kiasi cha Shilingi Bilioni 22.3 Ni kwa ajili ya shughuli za Miradi ya maendeleo.
Aidha jumla ya Shilingi Bilioni 69.6 ni makusanyo kutoka vyanzo vya mapato ya ndani ambapo ni fedha kwa ajili ya mishahara,matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.
Pia kiasi cha shilingi Bilioni 7 kinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye michango ya wananchi na wadau wa maendeleo katika kipindi cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ilipanga kutekeleza Miradi ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 56.1Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 33.7ambayo ni sawa na 70% ya jumla ya bajeti ya Miradi ya Maendeleo ni fedha ya mapato ya ndani na kiasi Cha shilingi Bilioni 22.3 ni Ruzuku kutoka Serikali kuu ambayo ni sawa na 30% ya jumla ya bajeti ya Miradi ya maendeleo ya Halmashauri.
Katika kipindi cha robo ya tatu kuanzia mwezi Januari Hadi Machi 2022,Halmashauri imepokea jumla ya fedha za Miradi ya Maendeleo kiasi Cha Shilingi Bilioni 11.6 kutoka vyanzo mbalimbali ambapo Shilingi Bilioni 8.6 zimepokelewa kutoka vyanzo vya ndani ya Halmashauri