Na Yusuph Digossi
Nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao inazidi kuwa finyu kwa upande wa matajiri wa Chamazi Azam.
Hali hiyo inakuja baada ya kuchezea kichapo cha 2-1 kutoka kwa vijana wa Mbeya City ambao walitumia vizuri Uwanja wao wa nyumbani Sokoine Jijini Mbeya.
Mbeya City waliandika bao la kwanza mnamo dakika ya 51 kupitia nyota wao Juma Shemvuri huku Beki Daniel Amoah akijifunga na kuipatia Mbeya City bao la pili dakika ya 83 na goli la Kufuatia machozi kwa upande wa Azam likifungwa na mshambuliaji wao Daniel Lyanga.
Baada ya kichapo hiki Azam Fc wanabaki na alama zao 32 huku wakikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Geita Gold ambaye ana alama 31, Namungo alama 30 na Kagera Sugar alama 29.
Ikumbukwe msimu ujao Tanzania itapeleka wawakilishi Wanne kwenye michuano ya kimataifa hivyo kocha wa Kikosi cha Azam ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha timu hiyo inashiriki michuano ya kimataifa.
Tags:
MICHEZO