Amref wakabidhi vifaa vya mazingira katika Jiji la Ilala

Mkurugenzi mkazi washirika la Amref Dr Florence Temu pamoja na Mkurugenzi wa miradi Dr Aisa Muya wakishuhudia Meya wa Jiji la Dar es Salaam  akikabidhi gari kwa kikundi cha wajisiriamali wa Kigilagila kwa lengo la kukusanyia taka na kuzichakata kuwa mkaa mbadala, gari hili pamoja na vifaa vingine kama Toyo (guta) 9, mashine 5 za kutengenezea mkaa, vifaa vya kukusanyia taka (dustbin) 80, pampu za maji taka 3, pamoja na vituo vya kunawia mikono 23 vimetolewa na shirika la Amref kwa vikundi vya ujasiriamali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa TAKA MALI NA AFYA.



Na Mwandishi wetu

Katika kuboresha Afya ya Jamii ya Tanzania kupitia mradi wa Taka Mali na Afya, Shirika la Amref Health Africa Tanzania limefanya makabidhiano ya vifaa vya mazingira katika Jiji la Ilala vikiwemo Toyo (Guta) 9, Mashine za Kutengeneza Mkaa 5, Dust bins(Vizolea taka) 80, Gari Suzuki Supper Cary, 1 , Pampu za Maji Taka 3 na Taulo za kike (Pads) pisi 750.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vya mazingira, Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk.Florence Temu alisema vifaa hivyo vya kuboresha mazingira vina thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 1;

"Kupitia mipango kazi iliyofadhiliwa , miradi iliweza kununua vifaa vya Kuboresha Mazingira vyenye thamani ya TSH Zaidi ya 1-bilion ili kuwezesha utendaji wa kazi Kwenye vikundi vya usafi na kuthibiti magonjwa ya mlipuko katika Jiji la Ilala na pia kuongeza kipato cha Wamama na Vijana"

Aidha Mkurugenzi huyo alifafanua juu ya vifaa ambavyo wamevikabidhi sehemu ambapo vitaenda kufanya kazi ili kudhibiti na kukinga Magonjwa;

"Toyo (Guta) 9 ambazo zitaenda Kigiragira Rafiki Mazingira, Kipawa Women Group, Mazingira, Uchumi na Jamii, Amani Development Group and Sauti ya Jamii Kipunguni, Mashine za Kutengeneza Mkaa 5, ambazo zitaenda Kigiragira Rafiki Mazingira, Kipawa Women Group, Mazingira, Uchumi na Jamii, Amani Development Group and Sauti ya Jamii Kipunguni"

"Vizolea Taka (Dust bins) 80 ambazo zitaenda Kigiragira Rafiki Mazingira, Kipawa Women Group, Mazingira, Uchumi na Jamii, Amani Development Group and Sauti ya Jamii Kipunguni.
Gari Suzuki Supper Cary , 1 ambazo zitaenda Kigiragira Rafiki Mazingira, Trash Pump  (Pampu Za Maji Taka) 3, Kigiragira Rafiki Mazingira"

Aliongeza kuwa "Vituo vya Kunawia Mikono 23, katika shule za Shule za Msingi: Vingunguti, Mtakuja, Yombo, Miembeni, Airwing, Minazi Mirefu, Gongo la Mboto JICA, Majani ya Chai, Bwawani, Yombo, Umoja, Muungano, Kiwalani, Kigilagila, Hekima, Mtakuja, Kichangani, Majohe na Mji Mpya, shule ya Msingi.  Vituo vya afya: Kiwalani, Vingunguti na Majohe na Taulo za Kike pisi 750, ambazo zitaenda Majani ya Chai, Buguruni Moto Mpya, Mwangaza, Majohe na Kigiragira"

Mkurugenzi huyo alisema wao kama shirika la Amref Health Africa Tanzania wanaahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na serikali kwa kufuata miongozo ya serikali na Wizara ya Afya ili kuboresha Afya ya Jamii ya Tanzania

Kwa upande wake Meya Wa Jiji la Ilala, Omary  Kumbilamoto aliwapongeza Amref kwa kuwa wadau muhimu wa kuhamasisha usafi na kulifanya Jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya sita Afrika;

"Tanzania imekuwa ni Jiji la 6 kwa Afrika ambapo Amref mpo ndani, hivyo nawashukuru sana kwa  hamasa mliyoitoa ya usafi na mazingira ili kuendelea kujikinga na kudhibiti mazingira"

Aidha Meya Kumbilamoto amevitaka vikundi vilivyonufaika na mradi kuvitunza vifaa hivyo ili kuendelea kutoa Hamasa kwa wadau kuendelea kuwashika mkono

 Mbali na hayo Meya Kumbilamoto amehamasisha umuhimu wa wananchi kushiriki katika zoezi la uwekezaji wa Anuani za makazi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu.



Post a Comment

Previous Post Next Post