Wafanyakazi Wanawake wa Jengo la Watoto Namba mbili wakijiandaa kupeleka mahitaji wodi ya watoto wenye Saratani. |
Wafanyakazi Wanawake wa Jengo la Watoto Namba mbili |
Wafanyakazi Wanawake wa Jengo la Watoto Namba moja
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Hospitali ya Taifa Muhimbili ( MNH)
Na Sophia Mtakasimba
Wafanyakazi Wanawake Hospitali ya Taifa ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameungana na Wanawake wote Duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake.
Katika Maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yalibeba kauli mbiu isemayo Kizazi cha haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu; Jitokeze kuhesabiwa, wanawake wa MNH wametumia siku hii kwa kutoa msaada kwa wahitaji katika Wodi za Wazazi , Wodi za Watoto wachanga, Wodi za Watoto wenye Saratani, pamoja na kutoa misaada kwa watoto waliohifadhiwa katika Mahabusu ya watoto Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
Chanzo Muhimbili Blog