MAYELE ATETEMA MAPEMA CCM KIRUMBA , MAPUMZIKO GEITA 0-1 YANGA SC

 


Na Yussuph Digossi- Sauti za Mtaa Blog 

Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara kati ya wenyeji Geita Gold dhidi ya Yanga hadi sasa ni mapumziko huku vinara wa Ligi kuu Tanzania bara Yanga Sc wakitoka kifua mbele kwa uongozi wa goli moja bila majibu katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza 

Bao la mapema kutoka kwa Kinara wa mabao Fiston Mayele ambaye alitumia vizuri makosa ya walinzi wa Geita Gold limewapa uongozi wananchi katika dakika 45 za kipindi cha kwanza 

Beki wa kulia wa Yanga, Paul Godfrey akiwania mpira na mlinzi wa kushoto wa Geita Gold Amos Charles katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara  katika dimba la CCM Kirumba Mwanza (Picha na mtandao wa Yanga )

Timu zote zilianza mchezo kwa kasi ya juu na kushambuliana kwa zamu, Geita Gold  walitengeza nafasi kadhaa  lakini mshambuliaji George Mpole alikosa umakini katika kumalizia 

Yanga imewakosa baadhi ya nyota wao muhimu katika kikosi cha kwanza akiwemo Saido Ntibanzokiza , Khalid Aucho, Farid Mussa , Djuma Shaban na Yacouba Sogne ambaye ni majeruhi wa muda mrefu. 

Paul Godfrey , Yasin Mustapha , Deus Kaseke na Salum Abubakar ( SureBoy) wameanza kwenye kikosi cha kwanza wakichukua nafasi za wachezaji waliokosekana

Kipindi cha Pili kinafuata , endelea kutembelea sautizamtaatz.blogspot.com kwa habari mbalimbali na matukio

Post a Comment

Previous Post Next Post