Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry Murro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha za kumalizia awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa Kukamilika kwa hatua ya kwanza ya jengo hili kunamanisha kusogezwa kwa huduma kwa wananchi hatua itakayorahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi uku jengo likiwa na mazingira rafiki kwa watu wenye changamoto ya ulemavu
"Namshukuru Mhe, Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha za kumalizia awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi" amesema Jerry Murro
"Kukamilika kwa hatua ya kwanza ya jengo hili kunamanisha kusogezwa kwa huduma kwa wananchi hatua itakayorahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi uku jengo likiwa na mazingira rafiki kwa watu wenye changamoto ya ulemavu"
Tags:
SIASA