Na Mwandishi wetu
Takribani Mapambano 16 ya ngumi yametambulisjwa rasmi hii leo kwaajili ya vita ya Fainali ya kumpata 'Champion wa Kitaa' itakayopigwa Uwanja wa Taifa Machi 20, 2022.
Katika utambulisho huo bondia Salehe Mkalekwa atapambana na Maono Ally wa Bagamoyo kwenye pambano kuu wakati Dullah Mbabe akikandana na Amour Sheikh Haji na Hassan Ndonga (tyson wa mbongo) akimuelekeza Ngumi Adam Mbega kwenye pambano la raundi 8.
Hata hivyo Mkufunzi wa Mabondia Kutoka Mabibo Kocha Christopher Mzazi amesema kutokana na kupewa majina tofauti kwenye ngumi, hivi sasa amepewa jina la Rais wa Urusi katika Pambano hilo.
Fainali za Champion wa Kitaa zinatarajiwa kupigwa 20 Machi 2022 katika Uwanja wa ndani wa Taifa (Indoor Stadium) ambapo baada ya Pambano hilo ni Maandalizi mema ya kuelekea Mkoani Morogoro kwaajili ya Pambano la Ubingwa Machi 26, 2022 Kati ya Twaha Kiduku Na Alex Kabangu wa Congo DR.