BALLON D'OR YAFANYIWA MABADILIKO KISA MALALAMIKO


Waandaaji wa tuzo ya Ballon d'Or wamepanga kuanza kutoa tuzo hizo kulingana na ubora wa mchezaji katika msimu husika tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo kulikuwa kinatazamwa kiwango cha nusu msimu kwa misimu miwili tofauti.

Tuzo za Ballon d'Or ambazo hutolewa na gazeti la Michezo Ufaransa mbali na kubadilisha muda wa kutazama ubora wa mchezaji pia wamepunguza waamuzi wa kuamua nani awe mchezaji bora.

Kabla ya mabadiliko hayo, kulikuwa na waandishi 170 ambao walikuwa sehemu ya jopo la maamuzi lakini sasa wamepunguzwa mpaka 100 kwa upande wa wanaume wakati katika jopo la kuamua nani awe bora kwa wanawake watakuwa 50.

 "Kabla tulikuwa tunatazama ubora wa nusu misimu miwili, hii itapunguza malalamiko", alisema Paschal Ferre mhariri wa gazeti hilo.

Mabadiliko hayo yanafuatia malalamiko ya msimu uliopita 2021 pale ambapo waandaaji walimpa nyota wa Paris St-Germain Lionel Messi tuzo wakati wengi wakidhani Mshambuliaji wa kimataifa wa Poland na Bayern Munich alikuwa akistahili zaidi tuzo hiyo.

Tuzo za msimu huu za Ballon d'Or zitatolewa mwezi Septemba au Octoba 2022 na kigezo kikubwa kitakuwa ni kiwango kizuri cha mchezaji kwenye msimu unaomalizika mwezi Julai.


Post a Comment

Previous Post Next Post