TAASISI ya Sekta Binafsi nchini imefanya mageuzi makubwa kwenye Katiba ili kuhimarisha ushiriki wa sekta binafsi nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu wa (TPSF),Raphael Maganga wakati akizungumza wahariri wa vyombo vya habari pamoja na Waandishi wa habari kuhusu maboresho saba ya katiba na kutanua wigo wa ushiriki.
Amesema katika maboresho yaliyopitishwa na mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Novemba 20 mwaka huu umebadilisha jina la taasisi hiyo kutoka Taasisi ya sekta Binafsi nchini na kuitwa Shirikisho la sekta Binafsi nchini(TPSF).
"Mabadiliko haya yamefanywa ili kuondoa mkanganyiko uliokuwepo kati ya wadau kwa taasisi yetu ni shirika la kutoa msaada badala ya sekta binafsi"Amesema Maganga.
Maganga amesema pia mkutano huo uliohudhuliwa na zaidi ya asilimia 70 ya wajumbe halali wa TPSF umefanya maboresho ya sasa ya shirikisho litakuwa linaongozwa na Baraza la Uongozi(Governing Council)ambayo litashughulika na wanachama na changamoto zao na pia chini ya kutakuwa na kamati tendaji itakayoundwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa maamuzi katika shirikisho lengo ni kutenganisha uwakilishi wa wanachama.
Aidha,Maganga amesema mabadiliko mengine nikuongeza kongani ambapo kutakuwa na kongani 25 sawa na wale wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC)badala ya kongani 10 za awali na kusema Uundaji wa Kongani zilitazamiwa sekta za kiuchumi na pia sekta mtambulika.
Mabadiliko mengine ni mfumo shirikishi ili kuhakikisha kuna mfumo shirikishi,na Shirikisho limeongeza wawakilishi na makundi muhimu ambayo hapo awali hayakuwepo kama vile wanawake,Biashara za vijana,ufugaji,uvuvi,afya,elimu na michezo ikiwemo kuongeza wawakilishi kutoka Zanzibar.
Mabadiliko katika uwajibikaji ambapo awali hapakuwa na kamati tendaji lakini katika mabadiliko haya ya katiba uwajibikaji utakuwa unasimamiwa na kamati tendaji ili kuhakikisha kunakuwa uendeshaji imara wa shirikisho