Serikali imesema Ushirikiano wa Tanzania na Nchi ya Jamhuri ya watu wa CUBA unamanufaa makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uzalishaji.
Hayo yamesemwa leo mkoa wa pwani na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberatus Malamula, wakati wa Halfa ya utiaji saini mkataba wa Uzalishaji mbolea na Viuatilifu hai katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa za kibiolojia.
Amesema ushirikiano wa Tanzania na Cuba ni muda mrefu na upo imara na kupelekea kuja kusaini mkataba wa kuendesha kiwanda cha kuzalisha dawa za kuua mazalia ya Mmbu,pamoja viwatilifu vya mbolea ambapo kitasaidia kuinua uchumi.
Aidha,Malamula amesema majadiliano yalifanyika kwa siku 15 kati ya timu kutoka Tanzania na Cuba na kupelekea kusainiwa kwa mkataba huo wa kihistoria.
Naye Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda Biashara,Exhaudi Kigahe,amesema serikali kupitia shirika la maendeleo la Taifa, (NDC) kukiwezesha kiwanda cha kuzalisha Viwadudu kupata soko la ndani na nchi na kukifanya kiwanda hicho kujiendesha kibiashara.
Tags:
HABARI