Meena: Sheria ya kuelekeza Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo kugawa matangazo inaleta ukakasi



Na Yusuph Digossi

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania Neville Meena amesema kuwa , hatua ya sheria kuelekeza Mkurugenzi wa Habari Maelezo kuwa mgawa matangazo ya serikali, inazidisha ukakasi.

 Meena, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika Kipindi cha Hali Halisi kinachorushwa na Kituo cha Radio Upendo leo tarehe 11 Agosti 2022, Jijini Dar es Salaam.

Meena ameeleza kuwa  Vyombo vya Habari vinajiendesha kwa matangazo na huu ni ushindani wa kibiashara, hivyo basi taasisi zote za serikali kulazimishwa kupeleka matangazo kwa Mkurugenzi wa Habari Maelezo ili ayagawe, sio sawasawa.

“Hii maana yake, kama chombo chako cha habari kimetafsiriwa kuandika kile ambacho serikali haikitaki, basi huwezi kupata matangazo. Huku ni kuua vyombo vya habari kiuchumi. Jambo hili liachwe kwenye ushindani wa kibiashara pekee,” amesema.

Hata hivyo Meena  amesema Watanzania wamerejea kufuatilia habari kutoka katika Magazeti, Radio na Televisheni.

"hali hii ilikuwa imepotea katika miaka michache iliyopita kutokana na tasnia ya habari kupita katika mazingira magumu" ameongeza

Kuhusu mazuri ya sheria ya habari Meena amesema kuna baadhi   ya vipengele vilivyobeba tasnia ya habari katika Sheria ya Habari ya Mwaka 2016,  ikiwemo  wanahabari kutambulika kama taaluma rasmi.

“Sio kila kilichokuwemo kwenye sheria iliyopo sasa hakifai, Hapana. Sheria hii ndio kwa mara ya kwanza imetambua habari kama taaluma na mwanahabari anafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment

Previous Post Next Post