KIKOSIKAZI KUFANYA MABORESHO MWONGOZO WA KITAIFA WA USAMBAZAJI WA TAARIFA ZA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU NCHINI




Dar es salaam - COSTECH 

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kimekutana  kwa siku tatu (3) kuanzia tarehe 9 - 11 Agosti 2022  kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa Kitaifa utakaotumiwa pia na Taasisi za Utafiti na Maendeleo pamoja na Taasisi za elimu ya juu zinazofanya utafiti - Jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kikao kazi hicho Kaimu Meneja wa Uhifadhi na Machapisho (DPM) kutoka COSTECH, Dkt. Wilbert Manyilizu amesema kuwa mwongozo huu ni muhimu kwa kuratibu upatikanaji, uchakataji, uhifadhi na usambazaji wa Taarifa za kitafiti na Kibunifu kutoka Taasisi za elimu ya juu na vituo vya utafiti.

"Wanaofanya utafiti wanakuwa na matokeo, na wanaofanya ubunifu wanakuwa na bunifu kadhaa, vyote viwili vinahitajika Kufika kwa utaratibu ulioratibiwa vizuri kwa walaji ikiwemo Serikali, hivyo mwongozo ni muhimu" amesema Dkt Wilbert


Dkt Wilbert ameongeza kuwa wadau wa uzalishaji wa matokeo ya tafiti na bunifu hizi  kitaifa wanatakiwa kusomana na taarifa zao zikae katika utaratibu mmoja au unaofanana. "Waratibu kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) tunapaswa kuwasiliana vizuri  kwa kupitia mwongozo na taasisi za vyuo vikuu pamoja na Taasisi za Utafiti na Maendeleo nchini"


Amefafanua kuwa, mwongozo huu utarahisisha uwiano wa uratibu katika kuishauri Serikali kwa masuala ya Sayansi,  Teknolojia na Ubunifu kupitia mfumo unaoratibu upatikanaji, uhifadhi, uchakataji na uwasilishaji wa Taarifa za Sayansi, Teknolojia  na  Ubunifu. 

"Tunaweka mwongozo utakaokuwa ni wa Kitaifa ambao taasisi hizi zitatengeneza miongozo ya kitaasisi inayotokana na mwongozo wa Kitaifa" alisema Dkt. Wilbert


Post a Comment

Previous Post Next Post